Monday, 28 May 2012
HURUMA YA KUKU KWA VIRANGA VYAKE
Asalam alykum, baada ya salaam nina mshukuru Allahsubhanahu wataala na rehma na amani zimuendendee kipenzi chake taalaa saYyidna muhammadin na family yake na maswahaba pia ni kawaida kumuona kuku akimuitiya kifaranga chakula wakati yeye mwenyewe ana njaa au akiwafunika viranga wake wasipate jua ilhali yeye anaunguwa na jua halikadhalika na mvua anafanya hivyo hivyo ili vifaranga visilowe na mara ngapi huyo kuku pia anajitiya hatarini ili vifaranga viwe salama?huruma iliyoje ushujaa ulioje. Lakini baada ya yote haya kifaranga kikikuwa hakina tena habari na mama mzazi yule na wala sijuwi kama kiliwahi kumuuliza mama ulinileaje? Alhamdu lillahi sisi wanaadaamu hukumbuka haya kuwa mama zetu waliyoyafanya haya yote na kupita haya walivumila kilio chetu cha usiku kucha walitusafisha tulipokuwa tukijichafua na nepi au kipande cha kanga. Kuku yeye hakubahatika kuchenji nepi na si pempazi. Hakika Allah hakumpendelea mama aliposema nani anafaa kumpenda zaidi mama yako na mama yako halafu baba yako Allah anatufundisha aliposema waqadhwaa rabbuka allaa. Taabudu illa iyyaahu wabilwalidaini i7saana imma yablughanna 3in-daka lkibaru a7huduma au kila huma falaa taqul lahuma uffin walaa tanharhumaa waqul lahumaa qaulan kariima wakhfidhlahuma jana7a dhulli min ra7matin waqul lahumaa qaulan kariima maana yake ni amehukumu ameamrisha ya kuwa asiabudiwe yeyote isipokuwa yeye tu Allah jalla jaluhu na kuwatendeya wema wazazi wako wawili wakifikiya uzee mmojawapo au wote wawili usiwaambiye nyamaza au usiwakaripie na uwaambie maneno mazuri, na uwashushie ubawa wa upole kama afanyavyo kuku na useme allh nakuomba uwasamehe na uwashushie rehma kama walivyonileya mimi wakati niko mdogo. Hassan Nurdin
Sunday, 27 May 2012
TUMSHUKURU ALLAH (ALHAMDULLILLAH)
Asalam alykum, Ukitaka kushukuru muangalie aliyechini yako halafu utaona Allah amekupenda kiasi gani, miguu miwili Alhamdulillah. Kuna wengine hawana macho, masikio, afya na hata chakula. Na vingine vingi ambavyo hatuwezi kuvifikiria. Allah ametuhakikishia ukishukuru (Allah) atakuzidishia. Alhamdulillahi. Hassan Nurdin
Friday, 25 May 2012
MCHANGO WA KUMFARIJI MFIWA
Asalaam Aleykum, Kuhusu mchango wa marehemu bibi yake Aziza Said. Tunaomba wanachama wote wajitolee kumchangia mfiwa ili aweze kupeleka chochote nyumbani ama kufanya hitma. Kama mnavyojua mfuko wetu hauwezi kumsaidia ila wanachama wanaombwa kumchangia chochote walichonacho. Kwa maelezo zaidi jinsi ya kutuma pesa wasiliana na Mwenyekiti Said Mchanjama. Ahsanteni. Katibu
Monday, 21 May 2012
ACCOUNT NUMBER
Asalaam Aleykum, Alhamdullillahi tumepata account, Islamic Bank of Britain wametukubalia kufungua account na wameshatuma account number pamoja na online banking account. Kuhusu Account number na maelezo zaidi ya jinsi ya kuweka ada ya kila mwezi mtayapata siku ya kikao ama wasilianeni na mweka hazina Fathiya Said Tel: 07878081832.. Ahsanteni.. Katibu
Friday, 18 May 2012
MKUTANO WELLINGBOROUGH
Asalaam Aleykum... Mkutano utafanyika tarehe 23/06/2012 na hii ndiyo address 5 Teal Lane, Wellingborough, NN8 4TT. Kwa maelezo zaidi ama ukipotea wasiliana na Mrs Mwanana Zuber Tel 07950515455/ 07950515450 Email mwanaana50@hotmail.co.uk. Ahsanteni na InshaAllah nawaombeni wanachama wote mfike, Katibu
KUHUSU SHADHILY BANK ACCOUNT
Naombeni msamaha kwa usumbufu uliojitokeza wa account number. Tulitegemea tutakuwa na account yetu ya chama haraka iwezekanavyo lakini tulipojaribu hatukufanikisha. Inshaalah tutajaribu Islamic Bank of Britain. Kwahiyo nitajaribu kumtumia kila mwanachama account number ya muda au ikiwezekana nije nayo kwenye kikao naomba maoni yenu? samahanini sana kwa usumbufu. Mweka hazina Fathiya Said Tel: 07878081832
BBQ
Wanachama wote tumekubaliana kufanya BBQ siku ya kikao, kwahiyo sote kwa pamoja tutakiwa kuchangia pesa za chakula kuanzia hivi sasa na mwisho wa kutoa mchango wa chakula ni tarehe 10 mwezi wa June. (Family £15 na single £10). Kuhusu jinsi ya kutuma hizo pesa kwenye account muone Ibrahim Salim ( Tel: 01908520736 au 07404489076) kwa maelezo zaidi na account number, Wabillah Tawufiq, Mwenyekiti Msaidizi Ibrahim Salim