Saturday, 30 June 2012

MWANACHAMA MPYA

Tunamkaribisha mwanachama mpya kwa jina Dida Haji, tumemkubali Bi. Dida kwa kipengele kipya cha chama "Viongozi wa chama wanao uwezo wa kumkubali ama kumkataa mtu yoyote anayetaka kujiunga na chama" Bi Dida Haji karibu Shadhily

Friday, 29 June 2012

ADA YA CHAMA NA MADENI

Asalaam Aleykum, wanachama wote tunasisitiza kwa yeyote ataeweka pesa kwenye account aweke reference jina lake ili tuweze kujuwa ni nani ameweka hizo pesa. Na kwa wote wanaodaiwa ada ya mwaka jana, naomba wamalizie deni, mnaturudisha nyuma. Shukrani, Mweka hazina, Fathiya Said

Thursday, 28 June 2012

ADA YA CHAMA

Je mwanachama apewe muda gani alipe Ada ya chama? Na sheria ipi ichukuliwe asipolipa Ada baada ya miezi 6. Naomba wanachama wachangie maoni yao

Wednesday, 27 June 2012

ADDRESS YA KURUDISHA FOMU

Kwa wanachama waliojaza fomu na wanataka kuzirudisha, Address yangu, 5 Waldstock house, 47 Carronade place, Thamesmead, SE28 0EE

Tuesday, 26 June 2012

MWANACHAMA MPYA

Mwanachama mpya anataka kujiunga na Shadhily jina lake Dida Haji anakaa Reading. Hivyo viongozi mnatakiwa kutoa maoni yenu kama mmemkubali ama mmemkataa.

NIDHAMU

Wanachama wote tunawakumbusha kwamba tunataka kutengeneza kipengele cha NIDHAMU katika katiba yetu, ili kiweze kuwa na MAAMUZI YAKE. Tunawakumbusha nyote kutoa mawazo yenu kwa pamoja, Mwenyekiti Msaidizi (Ibrahimu Salim)

SHUKRANI

ASALAM ALEYKUM Ndungu zangu.Mimi na family yangu tunatanguliza shukurani zetu zadhati kutupa nafasi ya kuwakaribisha kuwa pamoja. Na tunaomba radhi kama kulikuwa na upungufu wowote uliojitokeza. Ahsanteni sana, Bw. Zubery na family yake

Saturday, 23 June 2012

MKUTANO

Ahsanteni sana wanachama wote mliojitokeza kuja kwenye mkutano, kwa niaba ya Shadhily tunawashukuru Zubbery Qambertato'g na Mwanaana Zubbery Aboubakary kwa kutualika na kutukarimu. Mkutano ujao utafanyika Slough, tarehe 29 September 2012. Ahsante Fatouma Abdulsamad kwa kutualika. Vilevile tunawakaribishe wanachama watatu wapya, Fatma Abdulsamad, Mariamu Manding'o na Swada Karanda. Karibuni Shadhily, Katibu

Wednesday, 20 June 2012

MADA YA KIKAO TAREHE 23 JUNI

Mada ya kikao tarehe 23 juni

1. Ada ya chama. Kwa wale amabao hawajatimiza malipo. 30 minutes

2.utaratibu wa kusajili wanachama wapya. (katiba). 15 min. 

3. Mchango wa misiba wa ndugu (katiba). 15 minus

4. Account number na Standing Order. 15 min.