SHADHILY SOCIETY
Tuesday, 2 October 2012
SHUKRANI
Kwa niaba ya Shadhily Society naomba kutoa Shukrani za dhati kwa Hannat na Yusuph Family kwa kuwezesha kufanyika kikao chetu, kama kuna jambo tumewakosea tunaomba mtusamehe.. Ahsanteni
Saturday, 22 September 2012
MAJINA YA KHITMA
Asalaam Aleykum, naomba kila mwanachama aandike majina kwaajili ya kusoma Khitma. Ahsanteni
ADDRESS YA KIKAO
Asalaam Aleykum, kikao chetu kitafanyika tarehe 29/09/12, saa nane mchana, address 79 Roxwell road, Barking, Essex, IG11 0PS. Ahsanteni
MCHANGO WA CHAKULA
Asalaam Aleykum, nimeshatuma Account number kwaajili ya chakula kwa kila mwanachama, kwa wale wasiopata nijulisheni, naomba kila mwanachama achangie £15 Family na £10 single. Kuhusu Ada ya chama naomba kila mwanachama awe amemaliza Ada kabla ya kufika kwenye mkutano. Kuhusu Mada ya mkutano tutazungumzia kuhusu jinsi gani tutafanya kwa wale wanachama watakaoshindwa kutoa Ada, na kama mwanachama yoyote anayo MADA aseme ili tuweze kuijadili siku ya kikao. Ahsanteni
MADA YA KWENYE KIKAO
Asalaam Aleykum, Naomba wanachama wote mchangie MADA ambayo mnataka izungumzwe kwenye mkutano na pia kuhusu marekebisho ya KATIBA manataka kipengele gani kiangaliwe ama kibadilishe. naomba maoni yenu kabla ya mkutano. Ahsanteni
Saturday, 21 July 2012
DUA - MILTON KEYNES
Tutakuwa na mawaidha jumamosi tarehe 28 halafu tutakuftari sote hapa Milton Keynes, karibuni sana waislam wote, Yanaanza saa 10 jioni ni ndugu zetu wale wa London Arbil wa Taquwa wale ambao walikuwepo kwangu na dufu kama mnawakumbuka. Mwenyekiti Msaidizi, Ibrahim Salim
RAMADHAAN MUBARAK
Asalaam Aleykum, nawatakieni Ramadhaan Kareem ndugu zangu, naomba Mola awawezeshe mfunge Ramadhaaan kwa salama, naomba Mola awawezeshe muimalize Ramadhaan kwa salama, naomba Mola wakubalieni dua zenu na naomba Mola awasemehini makosa yenu, Ameen
Subscribe to:
Posts (Atom)