Monday, 28 May 2012
HURUMA YA KUKU KWA VIRANGA VYAKE
Asalam alykum, baada ya salaam nina mshukuru Allahsubhanahu wataala na rehma na amani zimuendendee kipenzi chake taalaa saYyidna muhammadin na family yake na maswahaba pia ni kawaida kumuona kuku akimuitiya kifaranga chakula wakati yeye mwenyewe ana njaa au akiwafunika viranga wake wasipate jua ilhali yeye anaunguwa na jua halikadhalika na mvua anafanya hivyo hivyo ili vifaranga visilowe na mara ngapi huyo kuku pia anajitiya hatarini ili vifaranga viwe salama?huruma iliyoje ushujaa ulioje. Lakini baada ya yote haya kifaranga kikikuwa hakina tena habari na mama mzazi yule na wala sijuwi kama kiliwahi kumuuliza mama ulinileaje? Alhamdu lillahi sisi wanaadaamu hukumbuka haya kuwa mama zetu waliyoyafanya haya yote na kupita haya walivumila kilio chetu cha usiku kucha walitusafisha tulipokuwa tukijichafua na nepi au kipande cha kanga. Kuku yeye hakubahatika kuchenji nepi na si pempazi. Hakika Allah hakumpendelea mama aliposema nani anafaa kumpenda zaidi mama yako na mama yako halafu baba yako Allah anatufundisha aliposema waqadhwaa rabbuka allaa. Taabudu illa iyyaahu wabilwalidaini i7saana imma yablughanna 3in-daka lkibaru a7huduma au kila huma falaa taqul lahuma uffin walaa tanharhumaa waqul lahumaa qaulan kariima wakhfidhlahuma jana7a dhulli min ra7matin waqul lahumaa qaulan kariima maana yake ni amehukumu ameamrisha ya kuwa asiabudiwe yeyote isipokuwa yeye tu Allah jalla jaluhu na kuwatendeya wema wazazi wako wawili wakifikiya uzee mmojawapo au wote wawili usiwaambiye nyamaza au usiwakaripie na uwaambie maneno mazuri, na uwashushie ubawa wa upole kama afanyavyo kuku na useme allh nakuomba uwasamehe na uwashushie rehma kama walivyonileya mimi wakati niko mdogo. Hassan Nurdin
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment